Course Description

Course Description

جـــــامعـــه سبهــــــــــــــــــــــــا

كلية اللغـــــــــــــــــــات

قسم اللغـــــات والدراسات الأفريقية

شعبة اللغة السواحيلية

البرنامج الدراسي للغه السواحيلية

CHUO KIKUU CHA SEBHA

KITIVO CHA LUGHA

IDARA YA LUGHA NA TAALUMA ZA KIAFRIKA

SEHEMU YA LUGHA YA KISWAHILI

MUHTASARI WA KOZI ZA PROGRAMU YA KISWAHILI

 

 

KOZI ZA MUHULA WA KWANZA  ( I )

 

SW 101 : MAZUNGUMZO

SAA KWA WIKI :4 

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kuamkia , kujitambulisha na

kueleza shughuli zake za kila siku katika mazungumzo .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1) Maamkizi ya : Habari …;_ jambo;Shikamoo katika vipindi mbalimbali vya siku.

(2)Kujitambulisha :jina,mahali unakoishi,uraia,kazi .

(3)Kumtambulisha mtu mwengine .

(4)Majina ya siku za wiki .

(5)Shughuli za kila siku .

(6)Kuhesabu tarakimu 1-100 .

   NB: Mambo ya kuzingatia :

      -Matamshi sahihi ya abjadi za Kiswahili.

      -Msamiati unaohusika kwa kila mada.

      -Viulizi vinavyohusika.

SW102 :UFAHAMU

SAA KWA WIKI :3

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujenga msamiati wa nyanja mbalimbali na kujibu maswali rahisi ya ufahamu .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Ujenzi wa msamiati kwa njia ya :

     a-Picha za vitu mbalimbali , k.m .

        Vitu vya darasani

        Vitu katika mazingira ya chuo

        Watu katika Familia

        Watu katika shuguli mbalimbali

        Wanyama , wadudu , mimea

        Vyombo vya usafiri

        Vyakula na milo n.k .

      b-Vitendo darasani vitakavyofanywa na mwalimu na wanafunzi pia , k.m .

          Kuandika , kusoma , kukaa , kusimama , kufundisha , kujifunza , kuingia ,                   kutoka , n.k .

 (2)Kujibu maswali ya   matini  zilizoandikwa kutokana na picha mbalimbali .

SW103 : MABARA YA LUGHA

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kusikilza, kutamka kwa usahihi sauti , maneno na sentensi fupifupi za Kiswahili .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Utamkaji wa Irabu za Kiswahili.

(2)Utamkaji wa konsonanti za Kiswahili.

(3)Utamkaji wa silabi za miundo mbalimbali ya Kiswahili.

    k.m . Irabu                                          = a , e , i , o , u

             konsonanti + Irabu                    = pa , ba , ka , ga , ja

             kons + Irabu +kons + Irabu      = baba , mama , dada

             kons + kons + Irabu                  = cha , tha , dha , sha

             kons + kons + kons + Irabu      = nywa , chwa , n.k .

(4)Utamkaji wa maneno mazima na sentensi fupifupi k.m . mtoto , pwani , ninasikia,yeye ni

     mwalimu .

SW104 : KUSOMA NA KUANDIKA

SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua abjadi ya Kiswahili kwa jumla na Kuandika herufi zake kwa hati ya Kirumi kwa unadhifu .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Kusoma herufi zote za Abjadi ya Kiswahili ( herufi A-Z )

(2)Kusoma kwa makini na kuzingatia

    a-Herufi A-G

    b-Silabi zinazoundwa kwa herufi A- G

    c-Maneno yanayoundwa kwa herufi A-G

(3)Kuandika kwa unadhifu :

     a-Herufi ndogo na herufi kubwa A-G

     b-Silabi zinazoundwa kwa herufi A-G

     c-Maneno yanayoundwa kwa herufi A-G

(4)Imla :Uandikaji wa sentensi fupifupi

     zinazozingatia herufi , silabi na maneno

      yanayotokana na herufi A-G

(5)Kusoma na kuandika tarakimu 1- 100 kwa

      maneno.

SW105 :SARUFI

SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua na kutumia Viwakilishi nafsi,Vitenzi vya msingi,Viulizi na Vimilikishi katika Mazungumzo ya kuamkia na utambulisho.

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Viwakilishi vya nafsi katika Umoja na Wingi

(2)Viambishi :

     a-Maana ya viambishi (maelezo ya jumla tu )

     b-Viambishi vya nafsi kwenye vitenzi katika Kukubali katika umoja na wingi i.e.   Ni- , U- , A-         – TU – , M- , WA-

    c- Viambishi vya nafsi kwenye vitenzi katika Kukanusha ktika Umoja na Wingi  i.e . Si- , Hu- ,           Ha- , – Hatu- Ham- , Hawa- .

(3)Vitenzi:

     a-Idadi ya nyakati katika Kiswahili : wakati uliopo , uliopita , ujao .

     b-Vitenzi mahsusi vya kozi hii ( katika wakati uliopo )

          (i)kitenzi KUNA katika Kukubali na Kukanusha

         (ii)kitenzi KUWA  katika Kukubali na Kukanusha.

        (iii) kitenzi KUWA NA  katika Kukubali na Kukanusha.

(4)Vivulizi wapi ? , Nini? , Nani? , Gani? , Ngapi? , Lini?

(5)Vimilikishi :-angu , -ako , -ake

KOZI ZA MUHULA WA PILI  ( II )

 

SW 201 : MAZUNGUMZO

SAA KWA WIKI : 4

MADHAMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kumudu mazungumzo akitumia nyakati

 mbalimbali , katika mazingira yanayomzunguka anapokutana na watu wengi.

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Maamkizi kwa watu wa rika mbalimbali , adabu za kuingia na kutoka katika   vipindi

 Mbalimbali vya siku .

(2)Mazungumzo katika sehemu zifuatazo :

     Dukani au Sokoni – kuuliza bei za vitu

     Darasani \ Chuoni

     Ofisi ya idara

     Nyumbani

     Njiani anapokutana na watu wengi  n.k .

(3)Shughuli zinazofanyka nyakati mbalimbali k.v . leo ,jana ,kesho .

(4)Watu wa familia moja na uhusiano wao

(5)Hali ya hewa

(6)Kusoma tarakimu 100 – 1000

(7)Kusoma saa kwa Kiswahili

SW202 : UFAHAMU

SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze Kusoma makala fupi na kujibu maswali juu yake .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Maana ya Ufahamu,aina na madhumuni yake

(2)Kusoma makala fupi zinazohusu :

    a-Hadithi fupi zenye mafunzo

    b-Maisha ya kila siku

    c-Matukio halisi mbalimbali

    d-Shughuli za watu mbalimbali

(3)Kuchambua msamiati uliotumika katika makala na kueleza maana yake

(4)Kujibu maswali ya ufahamu kutokana na taarifa iliyoandikwa katika makala tu .

SW203 : MABARA YA LUGHA

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kutamka maneno maalumu kwa usahihi pamoja na kusema kwa usahihi tungo – sentensi za viwango mbalimbali za Kiswahili .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Utamkaji wa maneno kamili

    a-Neno mojamoja :hewa , mwalimu , kitukuu

    b-Maneno ya muungano: kilembwekezi ,mwanajeshi ,mwendawazimu

    c-Sehemu mbalimbali za mwili za nje na za ndani

(2)Utamkaji sahihi wa :

    a-Majina maalumu (watu ,miji ,nchi ,n.k .)

    b-Majina ya siku za wiki na miezi

    c-Maneno ya kurudiarudia k.m . kidogokidogo ,kimbiakimbia ,mbalimbali n.k .

(3)Utamkaji sahihi (kwa kuweka mkazo au kupandisha sauti kwenye silabi) katika           sentensi  k.m . alikwenda ?      (swali)

                             alikwenda !      (mshangao)

                             alikwenda .      (taarifa)

                             barabara  (njia) , barabara (sawasawa)

SW204 : KUSOMA NA KUANDIKA

SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kukamilisha ujuzi wake wa kusoma na kuandika maneno ya Kiswahili yenye herufi H-Z .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Kusoma kwa makini na kuzingatia :

    a-Herufi H –Z

    b-Silabi zinazotokana na herufi H – Z

    c-Maneno yanayotokana na herufi H – Z

    d-Majina ya siku za wiki na miezi

(2)Kuandika kwa unadhifu :

    a-Herufi ndogo na herufi kubwa  H-Z

    b-Silabi zinazotokana na herufi   H-Z

    c-Maneno yanayotokana na herufi  H-Z

   d-Majina ya siku za wiki  na miezi

(3)Kuandika sentensi kwa njia ya imla kwa kutumia maneno yanayotokana na herufi zote A  Z

(4)Kusoma na Kuandika tarakimu 1- 1000 kwa maneno .

SW205 :SARUFI

SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kutumia Vitenzi katika nyakati mbalimbali katika kukubali na kukanusha , katika Umoja na Wingi na pia aweze kuzingatia kanuni za vitenzi vya silabi moja na kauli chache za sentensi .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Matumizi ya Viulizi : vipi? ( _ je? ) na kwa nini?

(2)Matumizi ya kiambishi tamati – ni kuonyesha wingi K.m .karibuni , kwaherini, shikamoni,n,k .

(3)Vitenzi katika nyakati mbalimbali katika Kukubali na Kukanusha.

(4)Kanuni ya kukanusha katika nyakati mbalimbali

     a-Vitenzi vyenye silabi moja  k.m .kuwa , kuja , kula , kunywa  .

     b-Vitenzi vyenye asili ya lugha za Kibantu na lugha  ya Kiarabu  k.m . lala,cheka,fikiri,jaribu .

 

 

 

 

KOZI ZA MUHULA WA TATU  ( III )

SW 301 : MAZUNGUMZO

SAA KWA WIKI : 4

MADHAMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kumudu mazungumzo katika mazingira ya shughuli mbalimbali , kueleza jinsi kitu kilivyo au kilipo , mavazi mbalimbali na vyakula mbalimbali .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Kujenga msamiati kuhusu :

    a-Sehemu / viungo mbalimbali vya mwili

    b-Vyakula mbalimbali

    c-Mavazi mbalimbali

      d-Vyombo na njia za usafiri

       e-Rangi mbalimbali – hasa rangi kuu

(2)Mazungumzo katika mazingira yafuatayo :

       a-Hospitali

       b-Benki / Posta

       c-Hotelini / mgahawani

       d-Kituo cha usafiri

        e-Kutafuta nyumba / chumba cha kupanga

(3)Kueleza mtu mwingine kuhusu :

        a-Sifa za kitu kilivyo : umbo , ukubwa , uzito , ufupi / urefu n.k .

        b-Mahali kitu kilipo : juu ya / chini ya ; mbele / nyuma ya ; karibu / mbali ya n.k

        c-Viwango :

                                    vizuri sana

                                    vizuri

                                    kiasi / wastani

                                   kidogo / kidogo sana

                                   vibaya /vibaya sana

(4) Kuhesabu 1,000 è 100,000

SW302 : UFAHAMU

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujibu maswali kutokana na habari aliyoisoma au kusikia .Pia aweze kuifasili alivyoielewa na kuifupisha .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Kusoma makala /Matini ndefu ( kuliko zile za SW202 ) zinazohusu :

    a- Habari za kawaida au za matukio

    b- Maelezo au maelekezo ya jinsi ya kufanya jambo

    c- Hadithi

    d- Maisha ya kila siku n,k .

(2)Kuchambua msamiati uliotumika na kueleza maana yake

(3)Kutokana na kusikiliza tu au Kusoma , mwanafunzi ajibu maswali yanayohitaji :

     a-Taarifa iliyotolewa waziwazi katika makala tu

     b-Fasili ya msomaji kwa taarifa ambayo haikuandikwa waziwazi katika makala

     c-Maoni ya msomaji

(4)Msingi ya kufanya ufupisho / muhtasri wa makala

SW303 : UTUNGAJI WA KUONGOZWA

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kutumia msaada atakaokuwa amepewa kukamilisha kazi anayotakiwa kutunga

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Maana ya Utungaji na dhima yake

(2)Aina za Utungaji _ wa kuongozwa na wa kujitegemea

(3)Mambo muhumu ya kuzingatia katika utungaji : i.e .

    a-Utafutaji wa mawazo , upangaji wa mawazo

    b-Utumiaji wa lugha fasaha kueleza mawazo

(4)Matumizi ya vituo na herufi kubwa

(5)Utungaji wa Mazungumzo

     a-Mazungumzo ya simu

     b-Mahojiano baina ya watu wawili katika mazingira mbalimbali

(6)Utungaji wa maelezo / maelekezo  k.m .

 a-Kadi mbalimbali  b-Taarifa fupifupi c-Matangazo mafupi  km. mchezo, biashara, kazi  n.k.

SW304 : KUSOMA NA KUANDIKA

SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kusoma na kuandika kwa upesi na kwa usahihi hadithi , habari na makala fupi

 

MADA ZA KUFUNDISHA :

 (1)Ujenzi wa msamiati kwa Kusoma vitabu vya mada mbalimbali  k.m. kilimo,ufundi , hadithi ,ukoo wa familia yake , historia ya kabila n. k .

(2)Kuimarisha kasi / wepesi wa kusoma na Kuandika kwa :

     a-Kusoma vitabu kwa zamu darasani

     b-Kuandika habari au matini kutoka kitabuni , kwa muda maalumu aliowekewa

     c-Kuandika matini kwa njia ya imla

(3)Kuandika hadithi / habari na kuisoma darasani

(4)Kusoma na Kuandika tarakimu 1,000 – 100,000 na pia namba zilizo katika vipimo                          mbalimbali  k.m . 21% ,6.05 , 1/3 , 5/8  n.k .

SW305 :SARUFI

SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua aina /kategoria za maneno ya Kiswahili na kuchambua Nomino na Vivumishi vya Kiswahili

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Aina / Kategoria za maneno ya Kiswahili kwa jumla

(2)Uchambuzi wa nomino :

     a-Maana na Aina za nomino

     b-Mitazamo ya uainishaji ngeli za nomino

        (i)Kigezo cha Kimofolojia (kuzingatia viambishi vya Umoja na Wingi)

        (ii)Kigezo cha Kisintaksia (Kuzingatia upatanisho)

(3)Ngeli za nomino na upatinishi wake kwenye:

     a-Kitenzi

     b-Vivumishi vya idadi na vimilikishi .

                     KOZI ZA MUHULA WA NNE  ( IV )

SW 401 : MAZUNGUMZO

SAA KWA WIKI : 4

MADHAMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujieleza kwa ufasaha katika kueleza matukio .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Kueleza matukio k.m .

     a-Katika kituo cha Polisi

     b-Jinsi ajali ilivyotokea

     c-Jinsi sherehe ilivyokwenda

     d-Mandhari ya Pwani

     e-Safari ya kitalii , likizo n.k .

(2)Kueleza namna ya kufanya au kushiriki katika shughuli  k.m .

     a-Kupika chakula fulani

     b-Kusafirisha kifurushi kwa posta  n,k .

(3)Kumwelekeza mtu njia

    a-Kwa maelezo : moja kwa moja ; karibu / jirani na ; pinda kulia / kushoto ;   mkabala na / mbele ya  n.k .

    b-Kwa dira ya ramani : Kaskazini / Kusini ; Mashariki / Magharibi

(4)Majira na nyakati za mwaka

    a-Hali ya hewa katika miezi inayohusika

    b-Mavazi , Vyakula na shughuli zinazofanywa

SW402 : UFAHAMU

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kusoma na kuelewa makala zilizo na semi maalumu kv.methali, vitendawili, nahau n.k  .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Makala ndefu zenye semi mbalimbali k.m.methali, vitendawili, nahau, sitiari, taashira, nk .            zinazohusu :

    a-Maisha ya kila siku

    b-Maelekezo / Maelekezo ya kutenda jambo

    c-Hadithi zenye mafunzo

    d-Matukio halisi  n.k  .

(2)Uchambuzi wa msamiati na maana za semi kama zilivyotumiwa katika makala

(3)Kujibu maswali yanayohitaji :

    a-Kuelewa taarifa iliyowaziwazi katika makala

    b-Kuelewa maana ya semi kama zilivyotumika

    c-Kutumia taarifa ambayo haikusemwa moja kwa moja katika makala

    d-Maoni ya msomaji

 (4)Uandikaji wa muhtasari / ufupisho wa habari kwa : aya baada ya aya na habari nzima  .

SW403 : UTUNGAJI

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze  kuwa mbunifu na kukamilisha

Utungaji wake kwa msaada mdogo sana .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Utungaji wa insha za maelezo

    a-Hatua za kupata mawazo yatakavyotumiwa

    b-Upangiliaji wa mawazo au hoja zilizopatikana

 (2)Utungaji wa barua za aina mbalimbali

    a-Barua za kirafiki

    b-Barua za kindugu

    c-Barua za kiofisi / suala rasmi

(3)Utungaji wa hadithi

     a-Kupanga mfuatano wa visa / matukio

     b-Haja ya kuzingatia funzo kuu , wahusika na Lugha yao

     c-Hadithi za Kuandika kutokana na mfululizo wa picha za tukio moja .

     d-Kukamilisha habari au hadithi iliyoanzwa

     e-Kuandika hadithi juu ya methali au nahau Fulani.

SW404 : KUSOMA NA KUANDIKA

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kupenda  kusoma na kuandika kutokana na tabia ya kuweka kumbukumbu ya yale anayosoma na kuandika

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Ujenzi wa msamiati kutokana na :

     a-Kusoma vitabu vya hadithi fupi na ndefu

     b-Magazeti au majarida

 (2)Kusoma vitabu au hadithi zilizo katika mfululizo fulani k.m.mchapishaji au            mwandishaji mmoja

 (3)Kuandika hadithi kwa ajili ya kuchapisha katika gazeti la darasa , chama cha kiswahili n.k .

 (4)Kusoma vitabu vya idadi iliyowekwa na kutoa ripoti kwa kila kitabu kuhusu :

     a-Muhtasari wa kitabu kilchosomwa

     b-Msamiati , semi au sentensi zilizomvutia .

SW405 :SARUFI

SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua upatanisho wa kisarufi

Kati ya Nomino na Vivumishi na pia Vitenzi pamoja na Dhana ya Urejeshi .

 

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Upatanisho wa kisarufi kati ya ngeli za Nomino na vivumishi vya

     a-Vivumishi vya sifa.

     b- _A unganifu.

(2)Aina za maneno zifuatazo :

     a-Nomino

     b-Vitenzi

    ch-Viwakilishi

     d-Vivumishi

(3)Matumizi ya AMBA – na upatinisho wake pamoja na viambishi mbalimbali vya O-Rejeshi

     kulingana na Ngeli ya Nomino inayohusika  k.m  . – cho- , – po – , -vyo- , – lo –  n.k  .

 

 

 

 

 

 

 

 

 

                     KOZI ZA MUHULA WA TANO  ( V )

SW 501 : Fonetiki

SAA KWA WIKI : 3

MADHAMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua Fonetiki ni nini na dhima yake katika taaluma ya Isimu .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Maana ya Fonetiki

(2)Dhima ya Fonetiki kama tawi la Isimu

(3)Matawi ya Fonetiki

(4)Misingi muhimu ya Fonetiki matamshi

  a-Ala za matamshi na kazi zake

  b-Aina za sauti zinazotamkwa : Irabu na Konsonanti

(5)Utamkaji wa sauti za Konsonanti kuzingatia

    a-Ala inayohusika

    b-Mahali panapohusika wakati wa kutamka

    c-Namna ya utamkaji (uhusishwaji wa mghuno )

(6)Mazoezi ya uwakilishaji vitamkwa katika maandishi ( kunukulu )

SW502 : UTANGULIZI WA FASIHI

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua maana ya Fasihi , chimbuko na tanzu zake pamoja na dhima yake .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Fasihi kwa jumla

   a-Maan ya Fasihi

   b-Fasihi kama sanaa

   c-Aina za Fasihi kuhusiana na lugha ya Kiswahili

 (2)Chimbuko la Fasihi : Nadharia za kidhanifu na kiyakinifu

 (3)Dhima ya Fasihi katika jamii

 (4)Tanzu za Fasihi : Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi

 (5)Misingi mikuu ya Fasihi Simulizi

    a-Maana ya Fasihi Simulizi

    b-Sifa / Vipengele vya Fasihi Simulizi

    c-Tanzu za Fasihi Simulizi

 (6)Hadithi

    Maana ya hadithi na vipengele vyake

SW 503 : TAFSIRI

SAA KWA WIKI : 3

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua tafsiri kama taaluma na aizingatie misingi yake anapofasiri .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Maana ya Tafsiri na historia yake kwa kifupi kama taaluma.

 (2)Umuhimu wa Tafsiri kwa jamii .

 (3)Aina za Tafsiri :

   a-Tafsiri ya neno kwa neno (sisisi )

   b-Tafsiri ya ujumbe lengwa (sabilia / huru )

 (4)Sifa za Tafsiri nzuri :

    a-Kuwasilisha ujumbe kutoka Lugha chasili (LC) kwenda Lugha Lengwa (LL)

    b-Kuzingatia umbo la makala ya LC na uzito uleule wa ujumbe

    c-Kuzingatia kiwango cha wanaolengwa kutumia tafsiri hiyo na malengo megine ya mwandishi.

    d-Kuzingatia uhalisi wa LC

 (5)Sifa za mfasiri mzuri

    a-Ujuzi wa lugha zote i.e . LC na LL

    b-Utaalamu wa mada / uwanja unaohusika

    c-Uaminifu : kwa ujumbe na uzito katika makala

 (6)Hatua za kufasiri :  mazoezi ya kufasiri sentensi au makala fupifupi

SW504 : UTUNGAJI

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kuandika insha za mjalada au za kutoa maoni

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Insha za kutoa maoni

    a-Kujibu barua katika gazeti

    b-Makala kuhusu mada maalumu

 (2)Uandikaji wa makala katika magazeti mbalimbali

 (3)Uandikaji wa hotuba mbalimbali ya kumkaribisha mgeni, kuagana na mgeni, ufunguzi wa     sherehe n. k  .

 (4)Uandikaji wa barua za kuanzisha mradi au kuomba uanzishwaji wa mradi .

SW505 :SARUFI

SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua utumiaji sahihi wa Viambishi Mtendwa katika kitenzi na pia Kauli za Kitenzi .

 

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Viambishi Mtendwa katika kitenzi :

    a-Viambishi mtendwa Nafsi katika Umoja na Wingi  i.e . –ni- ; -ku- ; -m- à -tu- ;

        -wa-(-ku- + -eni-) ;-wa-

    b-Viambishi mtendwa vya Nomino kadiri ya Ngeli . k.m . –u- ; -i- ; -ki- ; -vi-  n.k .

   ch-Nomino Mtenda na Mtendwa katikan sentensi (kubali na kukanusha).

(2)Kauli za kitenzi :

    Kauli ya kutenda                             k.m .   piga

    Kauli ya kutendea                                      pigia

    Kauli ya kutendwa                                     pigwa

    Kauli ya kutendesha (kusababisha)           pigisha

 (3)Uunganishaji wa kauli ili kuunda maneno mapya

     k.m  .  kutendea + kutendana = kupigana

                kujitendea + kutendea   = kujipigia  n.k  .

 

 

 

 

 

 

                     KOZI ZA MUHULA WA SITA  ( VI )

 

SW 601 : Fonolojia ya Kiswahili

SAA KWA WIKI : 3

MADHAMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kubainisha utamkaji wa irabu na pia kuhusisha  Fonolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili .

MADA ZA KUFUNDISHA :

 (1)Maana ya Fonologia .

 (2)Dhima ya Fonolojia .

 (3)Uhusiano na Tofauti baina ya fonolojia na Fonatiki .

 (4)Dhana muhimu za kuzangatiwa katika Fonolojia :

   a-Matamshi :

     – Utamkaji wa Irabu kwa kuzingatia :

           i-Hali ya midomo

          ii-Mwinuko wa ulimi

         iii-Msogeo wa ulimi

   b-Fonimu za Kiswahili

   c-Alofoni

   d-Silabi

   e-Mkazo

   f-Kiimbo

   g-Lafudhi

SW602 : FASIHI

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kufahamu tanzu zaidi za Fasihi  Simulizi na matumizi yake .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Ushairi Simulizi kama utanzu wa Fasihi Simulizi

   a-Nyimbo

   b-Ngonjera

   c-Majigambo

 (2)Semi kama utanzu wa Fasihi Simulizi

   a-Methali

   b-Vitendawili

   c-Nahau

   d-Misemo mbalimbali

 (3)Maigizo kama utanzu wa Fasihi Simulizi

   a-Maana ya maigizo

   b-Vipengele (vipera) katika maigizo

      i-Michezo

     ii-Vichekesho

    iii-Ngonjera  n.k  .

SW 603 : HITORIA YA  KISWAHILI

SAA KWA WIKI : 2

MADHAMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua asili ya lugha ya Kiswahili , kwa nini Kiswahili ni lugha ya  Kibantu na kukua kwake katika  karne mbalimbali.

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Asili ya Kiswahili ( Nadharia ya chimbuko lake )

  a-Kiswahili ni lugha inayotokana na Kiarabu

  b-Kiswahili ni lugha ya mseto wa Kibantu na Kiarabu

  c-Kiswahili ni lugha ya Kiafrika katika kundi la lugha za kibantu .

 (2)Ushahidi wa Kiswahili kuwa ni lugha ya Kibantu

   a-Ushahidi wa Fasihi Simulizi

   b-Ushahidi wa Kihistoria

   c-Ushahidi  wa Kiisimu

 (3)Kukua kwa Kiswahili katika vipindi mbalimbali :

   a-Kabla ya kufika wageni kutoka nje ya Afrika

   b-Wakati wa kipindi cha Waarabu ( karne ya 7-14 )

   c-Kipindi cha Wareno ( karne ya 15-17 )

   d-Kipindi cha Wamisionari ( karne ya 17-19 )

   e-Kipindi cha Wakoloni ( Wajerumani na Waigereza )

 (4)Lahaja za Kiswahili

SW 604 : MATUMIZI YA LUGHA

SAA KWA WIKI : 3

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kupata hazina ya kutosha kwa ajili ya kutumia Kiswahili kulingana na mazingira au shughuli mbalimbali.

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1) Dhima ya Lugha kwa jumla katika jamii.

 (2) Maana ya “matumizi ya lugha” na kazi yake kuu ya kupambanua utumiaji wa lugha kulingana       na:

  a- Mazingira ya Wahusika.

  b- Uhusiano baina ya wahusika.

  c- Mada ya Mazungumzo.

  d- Madhumuni ya Mazungumzo

 (3)Aina za Rejesta na matumizi yake

   a-Lugha ya mahakama

   b-Lugha ya hospitali

   c-Lugha ya hotelini

   d-Lugha ya dini

   e-Lugha ya mitaani (simo)

    f-Lugha ya kitarafa – inavyoweza kukua na kuwa lahaja ya kijiografia .

 (4)Aina za semi mbalimbali na matumizi yake

   a-Methali

   b-Vitendawili

   c-Nahau  n.k  .

SW605 :SARUFI

SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua kwa undani aina zaidi za   maneno , unyambulishaji wa maneno na uundaji wa maneno .

                                                                                                      

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Kauli za Vitenzi :

    Kauli ya kutendewa                     pigiwa

    Kauli ya kutendeka                      pigika

    Kauli ya kutendana                      pigana

    Kauli ya kujitendea                      jipiga

    Kauli ya rai ,ombi au amri           – pige

(2)Uungnishaji wa kauli ili kuunda maneno mabya :

      k.m : kutendea + kutendana = kupigiana

               kujitendea + kutendea = kujipigia n.k .

(3)Minyambuliko ya Nomino :

    a-Viambishi tamati           -i , -ji ,-zi , -shi (unisha mtu na shughuli)

    b-Kiambishi tamati          -o (kuonisha matokeo au chombo / kifaa)

   ch-Viambishi tamati         -vu na –fu (kuonesha mtu au tabia)

    d-Nomino tokana na Vitenzi vya asili ya Kiarabu (vinaviyochukua viambishi awali tu na                     vinavyochukua viambishi tamati tu)

(4)Mbinu za kuunda maneno:

    a-Kutukana na sauti, umbo au kazi ya kitu.

    b-Vitenzi kuwa Nomino.

   ch-Nomino kuwa Vitenzi.

    d-Vivumishi kuwa Vitenzi.

                     KOZI ZA MUHULA WA SABA  ( VII )

 

SW 701 : HISTORIA YA KISWAHILI

SAA KWA WIKI : 3

MADHAMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua  maendeleo ya Kiswahili tangu wakati wa harakati za kutafuta uhuru mpaka leo hii .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Matumizi ya Kiswahili wakati wa harakati za kutafuta uhuru

   a-Lugha iliyotumika katika mikutano ya hadhara

   b-Mojawapo ya lugha rasmi zilizotumika katika Baraza la kutunga                                                       Sheria(LEGCO) nchini Tanganyika

   c-Lugha iliyowaunganisha wananchi wa makabila mbalimbali

 (2)Kiswahili baada ya uhuru

    a-Lugha ya Taifa na mojawapo ya lugha rasmi 1963

    b-Sheria ya kuundwa kwa Baraza la Kiswahili la taifa (BAKITA) mwaka 1967

    c-Kuundwa kwa Baraza la Kiswahili la Zanzibar 1984

    d-Kuimarishwa kwa vyombo na vyama vinavyoshughulikia kukuza Kiswahili nchini Tanzania          na nje ya Tanzania .

 (3)Kiswahili katika vyombo vya kimataifa

    a-Umoja wa Afrika

    b-Jumuiya ya Afrika Mashariki

    c-Vyuo Vikuu vinavyofundisha Kiswahili

    d-Idhaa za redio zinazotangaza kwa Kiswahili n.k.

SW702 : FASIHI

SAA KWA WIKI : 3

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua misingi ya Fasihi Andishi na jinsi  ya kuihakiki .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Maana ya Fasihi Andishi na dhima yake

 (2)Uhusiano wa Fasihi Andishi Na Fasihi Simulizi na tofauti baina ya Fasihi hizo

 (3)Tanzu za Fasihi Andishi

    a-Riwaya

    b-Tamthilia

    c-Ushairi

 (4)Uchambuzi wa Tanzu za Fasihi Andishi

    a-Riwaya – maana yake na historia yake

    b-Historia fupi ya Riwaya ya Kiswahili

    c-Tamthilia – maana na historia yake

    d-Historia fupi ya Tamthilia ya Kiswahili

 (5)Fani na Maudhui katika Riwaya na Tamthilia

    a-Maudhui : Dhamira , Mtazamo , Ujumbe , Falsafa

    b-Fani : Wahusika , Muundo , Matumizi ya lugha

 (6)Uhakiki :

    a-Maana ya uhakiki na mhakiki

    b-Dhima ya uhakiki

    c-Hatua muhimu za uhakiki

NB : Vitabu mahsusi vya Riwaya na Tamthilia viteuliwe kwa ajili ya uchambuzi wa            kifasihi .

SW 703 : TAFSIRI

SAA KWA WIKI : 3

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kutumia misingi ya Tafsiri kufasiri kazi mbalimbali .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Mbinu mahsusi za kufasiri

  a-Kuongeza maneno ili ujumbe ueleweke

  b-Kupunguza maneno ili kuwasilisha ujumbe k.m .tafsiri za taaluma maalumu kv. sayansi, sheria      , uganga n.k

  c-Kuweka maelezo / ufafanuzi wa dhana maalumu , mazingira ya makala , n.k .

  d-Kuweka orodha ya maneno / istilahi maalumu zilizotumika katika tafsiri

 (2)Kuzingatia walengwa wa tafsiri

   a-Elimu yao /utaalamu wao

   b-Umri wao

   c-Makusudio yao kwa Tafsiri hiyo n.k .

   NB:Mazoezi ya kufasiri makala za aina / nyanja mbalimbali yatolewe kwa wanafunzi.Hatua muhimu za kufasiri zizingatiwe .

SW 704 : MATUMIZI YA LUGHA

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua tofauti kati ya Lugha ya Mazungumzo na Lugha ya Maandishi , chanzo cha makosa ya matumizi ya maneno na matumizi ya kamusi .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Lugha ya Mazungumzo na Lugha ya Maandishi

   a-Sifa za Lugha ya Mazungumzo

   b-Sifa za Lugha ya Maandishi

   c-Jinsi Lugha ya Mazungumzo na Lugha ya Maandishi zinavyokamilishana

 (2)Chanzo cha makosa ya maneno katika matumizi.

    a-Makosa kutokana na tofauti za maana za maneno k.m  .maneno yenye maana zaidi ya moja, maneno yanayokaribiana katika matamshi , visawe na vinyume

    b-Makosa ya Kisarufi

                                            i-Tungo zenye utata          ii-Upatanisho usio sahihi katika sentensi

(3)Matumizi ya kamusi

    a-Maana na umuhimu wa kamusi

    b-Aina za kamusi

    c-Muundo wa kamusi : Taarifa  muhimu katika kitomeo

    d-Utumiaji wa kamusi kutafuta maana za maneno mbalimbali .

SW705 :SARUFI

SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI: Mwanafunzi aweze kujua maana ya Sintaksia (Sarufi Miundo) na viwango vyake katika taaluma ya Sarufi .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Maana ya Sintaksia (Sarufi Miundo)

(2)Dhima ya Sintaksia katika Sarufi

(3)Viwango vikuu vya Sintaksia :

    a-Neno

    b-Kirai na aina zake

  ch-Kishazi na aina zake

   d-Sentensi na aina zake kwa kutumia mkabala wa Sarufi Mapokeo.

(4)Mikabala ya uchambuzi wa sentensi :

    a-Njia ya Matawi

    b-Njia ya Mishale

  ch-Njia ya Masanduku

SW 706 : MBINU ZA UTAFITI

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua misingi mikuu ya utafiti na dhima yake katika kazi ya utafiti .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Maana ya utafiti na dhima yake

   a-Tofauti ya kazi ya utafiti na kazi isiyo ya utafiti

   b-Dhima ya utafiti kama sehemu muhimu kwa mandeleo ya kazi mbalimbali

       k.m . elimu , lugha , teknolojia n.k  .

 (2)Vipengele muhimu vya utafiti

    a-kubaini tatizo / suala la kutafitiwa

    b-Umuhumu wa kufanya utafiti juu ya tatizo

    c-kutafuta utatuzi wa tatizo :

       i-Mbinu mbalimbali zitakazotumika

      ii-Watu ,vifaa , vitakavyotumika

     iii-Mahali utafiti utakakofanyika

     iv-Jinsi taarifa zilizokusanywa zitakavyochanganuliwa

 (3)Mapendekezo na maoni ya mtafiti baada ya kujua matokeo ya utafiti wake.

                       

 

 KOZI ZA MUHULA WA NANE  ( VIII )

SW 801 : UTAMADUNI

SAA KWA WIKI : 3

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujua vitambulisho vikuu vya Waswahili katika maisha yao ya siku kwa siku .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1) Maana ya utamadunin kwa jumla.

 (2) Nyanja kuu za utamaduni zinazowapambanua Waswahili

 a- Utaratibu wa uzazi i.e. kuzaliwa mpaka kupshwa tohara.

 b- Malezi ya watoto.

 c- Ndoa na harusi (ada zinazohusika)

 d- Kazi na shughuli za Waswahili.

 e- Misiba na mazishi.

 f- Dini

(3) Taratibu za sherehe za Waswahili.

 a- Ngoma za Waswahili wakati wa sherehe.

 b- Vyakula vya Waswahili wakati wa sherehe.

 c- Mavazi

(4)Itikadi na miiko ya Waswahili.

SW802 : FASIHI

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze  kujua muundo wa mashairi ya Kiswahili na kuyachambua .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Maana ya ushairi na dhima yake katika Fasihi

 (2)Historia fupi ya ushairi wa kiswahili

 (3)Aina za mashairi

   a-Mashairi ya kimapokeo

   b-Mashairi ya kisasa

 (4)Vipengele muhimu vya mashairi

   a-Maudhui : dhamira , ujumbe , mtazamo

   b-Fani:Muundo (ubeti , vina, mzima, kituo, muwala n.k ) matumizi ya lugha ya mkato na taswira

 (5)Uhakiki wa ushairi

   a-Maudhui na dhamira

   b-Fani : muundo na matumizi ya lugha

   c-Hatua za uhakiki wa ushairi

NB:Vitabu mahsusi vya mashairi ya muundo mbalimbali viteuliwe kwa ajili ya  uchambuzi wa kifasihi .

SW803 : TAFSIRI

SAA KWA WIKI : 3

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kutumia misingi ya Tafsiri kufasiri kazi mbalimbali .

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Matatizo ya kufasiri

   a-Tofauti za mifumo ya LC na LL – Sarufi na msamiati

   b-Tofauti za Utamaduni wa jamii ya LC na LL

   c-Semi maalumu k.m .methali , nahau , simo , vitedawili n.k .

   d-Tofauti ya nyakati ya mwandishi na mfasiri

NB:Mazoezi ya kufasiri makala za aina / nyanja mbalimbali yatolewe kwa wanafunzi.Hatua muhimu za kufasiri zizingatiwe .

SW 804 : MATUMIZI YA LUGHA

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze kujenga msamiati / istilahi za nyanja mbalimbali, kujua dhima ya ishara katika mawasiliano na kutumia hazina hiyo katika stadi za midahalo

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Ujenzi wa msamiati kutokana na :

    a-Kazi mbalimbali za watu

    b-Sifa maalumu za watu k.m .mziwanda , kifungua mimba n.k .

    c-Maumbo ya vitu mbalimbali

    d-Sehemu mbalimbali za miili ya wanyama n.k .

(2)Uundaji wa istilahi 

    aMaana na dhima ya istilahi

    b-Mbinu mbalimbali za kupata / kuunda istilahi

 (3)Utumiaji wa ishara kama njia ya mwasiliano

    a-Alama na matumizi yake

    b-Picha na michoro k.m . mabango ya kampeni Fulani

 (4)Stadi za mdahalo

   a-Kuelewa mada

   b-Kukusanya / kuunda hoja

   c-Mpangilio wa hoja

   d-Kutumia mitindo mbalimbali wakati wa kutoa hoja / ujumbe  n.k .

SW805 :SARUFI  SAA KWA WIKI : 4

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi ajue taaluma ya Semantiki kama tawi la isimu na dhima yake katika lugha

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Maana ya Semantiki na historia yake kwa kifupi

 (2)Umuhimu wa Semantiki katika lugha

 (3)Viwango vya Semantiki :

    a-Kiwango cha Neno (Kiwango cha kileksia)

        i-Nadharia za Maana ya Maana

       ii-Aina za Maana (ya msingi na ya ziada)

iii-Uhusiano baina ya maana : k.m . Polisemia , Sinonimia ( Visawe) Homonimia,  Antonimia(Vinyume)  Haiponimia(Udarajia)

b-Kiwango cha Sentensi (Kiwango cha kisarufi)

       i-Maana kutokana na uamilifu wa neno katika sentensi km.Mtenda, Mtendwa,           Kifaa , Msisitizo n.k .

     ii-Utata wa sentensi kutokana na umbo la nje.

(4)Uhusiano wa Semantiki na tanzu zingine za isimu k.m. Fonetiki, Mofolojia na Sintaksia .

SW806 : UTAFITI  ( KAZI MAALUMU )

SAA KWA WIKI : 2

MADHUMUNI YA KOZI : Mwanafunzi aweze Kuandika kwa unadhifu kazi maalumu kutokana na Utafiti aliofanya    

MADA ZA KUFUNDISHA :

(1)Upangaji wa sura zitakazoandikwa

     k.m. Sura ya 1 : Utangulizi

             Sura ya 2 : Mapitio ya maandishi mbalimbali

             Sura ya 3 : Njia za kukusanya data

             Sura ya 4 : Matokeo

             Sura ya 5 : Hitimisho , Maoni na Mapendekezo

 (2)Upangaji wa Vipengele vya kila sura

 (3)Uandikaji wa Marejeo

    a-Ndani ya kazi yenyewe

    b-Kwenye kurasa maalumu mwishoni mwa ripoti

 (4)Upangaji wa Viambatisho

 (5)Uandikaji wa kurasa tngulizi kabla ya ripoti yenyewe k.m.

              a-Jina la mada na mwandishi

              b-Kiapo

              c-Tabaruku

              d-Shukurani

              e-Kifupisho cha ripoti

              f-Orodha ya yaliomo na kurasa zake

             g-Marejeo

             h-Viambatisho k.m. picha , rasmi , maswali , n.k .