Usawiri wa Nafasi ya Mwanamke katika Tamthiliya ya Kiswahili "Tamthiliya ya Alikiona kama mfano"

Main Article Content

IsmahanIsmahan Abulkasim Issa Massuod

Abstract

Makala hii inalenga kuchunguza usawiri wa nafasi ya mwanamke  katika tamthiliya ya Kiswahili "Tamthiliya ya Alikiona kama mfano" Katika kufanikisha lengo hili, tulichambua usawiri wa nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Alikiona na kuelezea uhalisia wa nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Alikiona kwa jamii ya leo. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa usawiri wa mwanamke unajitokeza katika maeneo ya mwanamke ni uzinzi, mwanamke ni mtu wa hila na ghilba, mwanamke ni mpenda ufahari, mwanamke ni muongo, mwanamke na mmbeya, mwanamke na ujanja, mwanamke ni mtunza kumbukumbu, mwanamke ni stara, mwanamke ni mpenda kupigwa na mwanamke ni mtoa matusi. Usawiri huu wa nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Alikiona umethibitika kuwa na uhalisia katika maisha halisi ya jamii ya Watanzania ambapo mwanamke halisi anafanana na mwanamke ambaye anatajwa katika tamthiliya. Wapo wanawake kadhaa ambao wamekuwa na sifa kama hizo za mwanamke anayetajwa katika Alikiona.

Downloads

Download data is not yet available.

Article Details

How to Cite
Massuod, I. A. I. (2024). Usawiri wa Nafasi ya Mwanamke katika Tamthiliya ya Kiswahili "Tamthiliya ya Alikiona kama mfano". Journal of Human Sciences, 23(1), 35–40. https://doi.org/10.51984/johs.v23i1.2583
Section
Articles