UCHAMBUZI WA FASIHI ZA KIFUNGWA: MFANO KUTOKA HAINI

Authors

  • Ismahan Abulkasim Issa Department of African Languages and Studies, Faculty of Languages, Sebha University
  • Jalgham Abuazuom Emhemed Ali Department of African Languages and Studies, Faculty of Languages, Sebha University

DOI:

https://doi.org/10.51984/johs.v24i1.3704

Keywords:

Fasihi, Nadharia, Ufungwa, Jela, kazi

Abstract

Makala hii inahusu uchambuzi wa fasihi za ufungwa ambazo zimehakiiwa kwa mkabala wa pendekezwa wa nadharia ya ufungwa. Ufungwa kama nadharia pendekezwa ya kuhakikia kazi za kifasihi za Ufungwa. Dhana ya Ufungwa hufasiliwa kama hali ya mtu kuwekwa jela akitumikia kifungo. Fasihi ya Ufungwa ni dhana ngeni ya kifasihi inayorejelea maandiko au kazi zote zinazohusu maisha ya jela au mahabusu. Aghalabu kazi za ufungwa huhusishwa na miktadha ya maisha ya mwandishi wa kazi husika.

Kimazoea nadharia huendelea kutumika kuhakiki kazi za kifasihi kwa muda mrefu hata kama nadharia hiyo inapwaya. Hivyo, kwa upungufu huo mhakiki hujikuta akitumia nadharia zaidi ya moja kuhakiki kazi husika ili kuweza kukidhi malengo yake. Hata hivyo, hali hii inapaswa kubadilika kutokana na kasi na mitindo na kumbo mpya za kifasihi zinazoibuka hususani Fasihi ya Ufungwa. Kutokana na mabadiliko haya nadharia kongwe hujikuta hazina budi kupisha nadharia mpya ili ziendelee kuhakiki kazi mbalimbali zinazoibuka.

Oswald, anaona kazi za ufungwa zinaweza kuhakikiwa kwa nadharia ya Kuwako‟ (Existentialism), Uhistoria Mpya‟, na „Elimu Mitindo‟ Pamoja na muongozo huu lakini tunaona bado nadharia hizo pia hazijitoshelezi kuhakiki kazi ya ufungwa kwa ujumla wake. Badala yake, zitajikita katika kuchambua tukio mojamoja. Hivyo, tunaona jinsi tunavyopata shida tunapotakiwa kuchambua kazi za ufungwa. Hatuwezi kuongozwa na nadharia moja ama mbili zikatosheleza, bali tutajikita katika kutumia mzigo wa nadharia katika kuhakikia kazi moja. Kwa upungufu huu, makala hii itajaribu kupata suluhisho la nadharia ambayo ingeweza kuhakiki kazi za ufungwa kwa jumla pasi na kutumia rundo la nadharia katika kazi moja. Makala hii itafafanua jinsi nadharia pendekezwa ya Ufungwa itakavyojitosheleza kuhakiki kazi za ufungwa ikidondoa mihimili ya nadharia hiyo na matumizi yake.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2025-06-30

Issue

Section

Articles

Categories

How to Cite

UCHAMBUZI WA FASIHI ZA KIFUNGWA: MFANO KUTOKA HAINI . (2025). Journal of Human Sciences, 24(1), 237-241. https://doi.org/10.51984/johs.v24i1.3704

Similar Articles

1-10 of 24

You may also start an advanced similarity search for this article.