Lugha Na Utamaduni: Uhusiano Wa Kisemantiki Katika Methali Za Kiswahili Na Kiarabu

Main Article Content

Abdellatif laabidi

Abstract

Makala hii imejikita katika mtazamo mtambuka na linganishi wa taaluma za lugha na utamaduni. Lengo la makala hii ni kuonesha uhusiano kati ya utamaduni wa Mwarabu na Mswahili kupitia lugha ya Kiswahili na Kiarabu katika nyanja ya kiisimu. Inaainisha mfanano baina ya methali za Kiswahili na Kiarabu katika mawanda ya semantiki. Kwa kutumia nadharia ya Grice ya semantiki makusudio, makala hii inajenga hoja kuwa methali za Kiswahili na Kiarabu zinathibitisha uwepo wa uhusiano ambao unaashiria na kuthibitisha mwingiliano wa kitamaduni baina ya Waswahili na Waarabu. Imebainika kuwa methali za pande zote mbili zinashiriki mantiki kimuktadha kwa kuzingatia lengo la ujumbe wa methali husika. Data ya makala hii ilikusanywa kupitia mahojiano pamoja na upitiaji matini. Sehemu kubwa ya data iliyokusanya inajumuisha methali za Kiswahili na Kiarabu pamoja na maana zake. Pia wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili na Kiarabu wapatikanao jijini Dar es Salaam, Tanzania walihusika katika mahojiano. Walihojiwa juu ya maana na matumizi ya methali hasa katika nyanja ya familia na mfumo wa haki. Makala hii pamoja na umuhimu wake kitaaluma, inaweza kutumika katika kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni na hata diplomasia baina ya Tanzania na mataifa ya Kiarabu.

Downloads

Download data is not yet available.

Article Details

How to Cite
laabidi, A. (2024). Lugha Na Utamaduni: Uhusiano Wa Kisemantiki Katika Methali Za Kiswahili Na Kiarabu. Journal of Human Sciences, 23(1), 182–188. https://doi.org/10.51984/johs.v23i1.3024
Section
Articles