Malezi Ya Watoto Enzi Za Wazanzibari Wa Kale
Main Article Content
Abstract
Maandalizi ya malezi ya watoto enzi za wazanzibar wa kale yalianza mapema mara mwanamke anapochukuwa uja uzito. Mjamzito aliandaliwa mambo maalumu kama chakula chake , nguo , sehemu maalumu ya kukaa ili ajifungue salama na kuanza kumlea mwana. Naye mwana aliyezaliwa alikuta ameshaandaliwa mambo yanayomhusu na hupokelewa kwa dua na shangwe toka kwa wanafamilia na wengine. Alipelekwa madrasa kujifunza kusoma kurani tukufu na elimu nyingine za maadili ya kiislamu ambazo ndizo zilizokuwa msingi mkuu wa kurekebisha maadili yake. Pamoja na haya alifundishwa kivitendo kuheshimu wengine katika jamii kwa kadri ya hadhi zao . Alipelekwa shule kujifunza elimu za mazingira na sayansi mbali mbali pamoja na lugha za kigeni na sanaa mchanganyiko ili kumjenga kimaarifa na kumwandaa kuitumikia jamii. Watoto walipobaleghe walipelekwa jandoni, kwa watoto wa kiume, na unyagoni kwa watoto wa kike. Huko walifunzwa namna ya kukabiliana na mabadiliko yaliyojitokeza katika miili yao na namna ya kuishi katika jamii wakiwa watu wazima tayari kuanzisha familia pindi muda utakapowadia. Malengo makuu ya malezi haya yalikuwa kumtayarisha mtoto kuishi maisha ya maadili mema katika jamii na kutoa mchango wake kwa kadiri ya nafasi yake katika jamii husika.
Downloads
Article Details
Plagiarism policy
Sebha University Journal respects intellectual property and aims to protect the original work of authors applying for publication. In general, the laws of the magazine are inconsistent with scientific articles that contain stolen materials and are not bound by the standards of quality, research and innovation. Applicants for publication to the journal must adhere to ethical standards and refrain from plagiarism in any way. In the event that any plagiarism or scientific theft of an article submitted for publication is found, the journal will contact the author to provide their interpretation within two weeks of its date, after which it will be referred to the relevant committees formed for this purpose to take strict measures. about that. In general, the journal’s license allows the citation of the content published on its website and the download of all files.