Baadhi ya Mbinu za Kifani katika Riwaya ya Kiswahili "Riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman kama mfano"

Main Article Content

Jalhgam Abu Azuom

Abstract

Kazi ya fasihi ikiwemo riwaya huundwa na fani na maudhui, ambavyo kwa pamoja ndivyo hutupatia kazi inayoitwa fasihi. Fani huundwa na vipengele kama vile wahusika, mtindo, mandhari, muundo na matumizi ya lugha. Vipengele hivi hutumiwa na waandishi kwa namna tofauti tofauti kulingana na ujuzi na welei wao. Kwa upande wa maudhui ni jumla ya mawazo makuu yanayoelezwa na mwandishi au msimulizi wa kazi ya fasihi na kutaka hadhira yake ipate .


kazi huu ulikusudiwa kufanywa kwa nia ya kuchunguza dhamira mbalimbali ambazo zinawasilishwa na Mohamed Suleiman katika riwaya yake ya Kiu. Kupita riwaya hii tumeainisha na mbinu za kifani zilizotumiwa na mwandishi katika kuibua dhamira ndani ya riwaya hiyo.


Kiu ni riwaya ya Kiswahili inayoelezea hadithi ya Bahati, kijana mwanamke aliyelelewa akaleleka na sasa anakutana na Idi, mwanaume laghai. Iddi hakawii kumzonga Bahati kwa kamba ya mapenzi ya uwongo. Bahati akiwa kalowa mapenzi hajijui hajitambui, anang’amua kuwa Iddi kwa kweli hampendi yeye, bali nafsi yake mwenyewe, na yeye Bahati ni chombo tu cha kutimiza shauku zake za kilimwengu. Kama ndege aliyenaswa katika ulimbo, jitihada zake za kujipatia nusura zinamletea angamio.

Downloads

Download data is not yet available.

Article Details

How to Cite
Abu Azuom , J. (2023). Baadhi ya Mbinu za Kifani katika Riwaya ya Kiswahili "Riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman kama mfano". Journal of Human Sciences, 22(1), 82–86. https://doi.org/10.51984/johs.v22i1.2521
Section
Articles