Ufeministi Unavyopingana Na Uislamu Kuhusu Mwanamke

Main Article Content

جابر الزروق

Abstract

Makala imejadili namna Nadharia ya Ufeministi inavyopingana na dini ya Uislamu juu ya nafasi ya mwanamke. Aidha makala imebainisha baadhi ya aya za Kurani tukufu na hadithi za Mtume Muhammad SAW zinazodaiwa kuendeleza unyanyasaji na ukandamizwaji wa mwanamke. Ukandamizwaji wa mwanamke hasa katika kipengele cha dini na ndoa umekua ukijadiliwa na kuzua migongano ya kihakiki. Suala la umiliki wa mali limeonekana kwa kiasi kikubwa kumtenga mwanamke kiuchumi. Nadharia ya Ufeministi wa Kiislamu imetumika katika kulijadili suala hili. Vilevile nadharia ya Mwitiko wa Msomaji na Uhalisia wa kijamii zimetumika katika kuzihakiki kazi za kifasihi. Aidha makala inaazimia kufuta fikra zilizo zoeleka kuwa, kinachotendeka katika nchi za magharibi ni kigezo cha taaluma na maisha bora ya ulimwengu.

Downloads

Download data is not yet available.

Article Details

How to Cite
الزروق ج. (2024). Ufeministi Unavyopingana Na Uislamu Kuhusu Mwanamke. Journal of Human Sciences, 23(2), 101–106. https://doi.org/10.51984/johs.v23i2.3141
Section
Articles
No Related Submission Found