Changamoto za Kuhifadhi Lugha ya Kiswahili Katika Zama za Utandawazi

Authors

  • Jalgham Abuazuom Emhemmed Ali Department of African Languages and Studies, Faculty of Languages, Sebha Universty

DOI:

https://doi.org/10.51984/johs.v24i2.4294

Keywords:

Changamoto, Elimu, Teknolojia, Utandawazi, zama

Abstract

Utafiti huu unachunguza changamoto zinazolikabili lugha ya Kiswahili katika zama za utandawazi, ambapo maendeleo ya kijamii, kiutamaduni na kiteknolojia yameathiri pakubwa matumizi na hadhi ya Kiswahili. Lugha za kigeni kama Kiingereza na Kifaransa zimepewa kipaumbele katika sekta za elimu, biashara na teknolojia, hali inayosababisha Kiswahili kupoteza nafasi yake ya hadhi. Changamoto nyingine ni uhaba wa rasilimali za lugha, ikiwemo kamusi, vitabu vya kitaaluma na maandiko ya kidijitali, jambo linalodumaza maendeleo ya kitaaluma na kitaifa ya Kiswahili. Utafiti umetumia mbinu ya kimaelezo (descriptive method) na kuongozwa na nadharia ya soshilinguistiki, ili kuchunguza uhusiano kati ya lugha na muktadha wa kijamii na kimataifa. Data zimekusanywa kupitia uchambuzi wa maandiko, makala za kitaaluma, mahojiano na hojaji, hatua iliyowezesha kupatikana kwa mtazamo mpana na wa kina kuhusu changamoto zinazolikabili Kiswahili. Matokeo yanaonyesha kuwa bila jitihada za makusudi kutoka kwa serikali, vyombo vya habari na jamii, Kiswahili kiko katika hatari ya kudhoofika zaidi. Hivyo, kuna haja ya mikakati ya pamoja ya kukilinda, kukiendeleza na kukipa nafasi pana kama lugha ya taifa na pia lugha ya kimataifa.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2025-10-02

Issue

Section

Articles

Categories

How to Cite

Changamoto za Kuhifadhi Lugha ya Kiswahili Katika Zama za Utandawazi. (2025). Journal of Human Sciences, 24(2), 193-197. https://doi.org/10.51984/johs.v24i2.4294

Similar Articles

1-10 of 49

You may also start an advanced similarity search for this article.