Chimbuku la Ushairi wa Kiswahili

Authors

  • Bubaker Owhida Ahmed Owhida Department of African Languages and Studies, Faculty of Languages, Sebha

DOI:

https://doi.org/10.51984/w3qyp205

Keywords:

Mamboleo, mapokeo, Mizani, Urari, Ushairi, Vina, Wanasasa

Abstract

Ushairi ni utanzu muhimu wa fasihi katika jamii nyingi hususani za Kiafrika katika kupitisha maudhui mbalimbali ya jamii. Ushairi wa Kiswahili ndio utanzu mkongwe zaidi wa fasihi. Ushairi huu umepitia mabadiliko mengi, mabadiliko haya yapo katika upande wa maudhui, miundo na mitindo ya lugha inayotumiwa, Mashairi hayo yamepitia hatua za usimulizi, maandishi ikiwa awali ni kwa hati ya Kiarabu na baadaye hati ya Kirumi/ Kilatini. Makala hii katika sehemu yake ya kwanza inajadili dhana ya ushairi ya Kiswahili kwa mitazamo ya wataalamu mbalimbali wa mikabala miwili tofauti yaani mkabala wa kimapokeo au wanamapokeo na mkabala wa kimamboleo au wanasasa Sehemu ya pili ya makala hii inatalii chimbuko la ushairi wa Kiswahili na inajadili hoja mbili, kuhusu mada hii na ubora na udhaifu wa kila hoja. Hoja ya kwanza inadai kuwa; chimbuko la ushairi wa Kiswahili ulitokana na ujio wa Waarabu. Na hoja ya pili inasema kuwa; chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la jamii ya waswahili wenyewe.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2026-01-28

Issue

Section

Articles

Categories

How to Cite

Chimbuku la Ushairi wa Kiswahili. (2026). Journal of Human Sciences, 25(1), 65-67. https://doi.org/10.51984/w3qyp205