Kushamiri Kwa Dhamira Ya Mapenzi Katika Muziki Wa Bongofleva: Dalili Za Kudumaa Kwa Sanaa

Main Article Content

Mohamed Yonis Khalifa

Abstract

Sanaa ni taaluma pana inayojumuisha tanzu mbalimbali lakini malengo ya tanzu hizi hufanana. Mfano; muziki, filamu, ushairi, uchoraji, na uchongaji ni miongoni mwa tanzu mbalimbali za sanaa zinazotofautiana kimuundo lakini zote hulenga aidha katika kuelimisha, kuburudisha, ama kudumisha utamaduni wa jamii husika. Makala hii inachunguza kushamiri kwa dhamira ya mapenzi katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania maarufu kama Bongofleva. Ni dhahiri kuwa kazi moja ya fasihi inaweza kubeba zaidi ya dhamira moja katika maudhui yake kulingana na mambo mahususi yanayojadiliwa katika kazi hiyo. Katika zama za hivi karibuni, muziki wa kizazi kipya wa Bongofleva umekuwa ukitawaliwa na dhamira ya mapenzi pekee kwani wasanii wengi wamekuwa wakirekodi nyimbo zilizosheheni kwa asilimia kubwa maudhui ya kimapenzi. Aidha, neno ‘mapenzi’ katika makala hii linamaanisha mahusiano ya kimapenzi baina ya mwanaume na mwanamke

Downloads

Download data is not yet available.

Article Details

How to Cite
Khalifa م. ي. . (2021). Kushamiri Kwa Dhamira Ya Mapenzi Katika Muziki Wa Bongofleva: Dalili Za Kudumaa Kwa Sanaa. Journal of Human Sciences, 20(2), 8–12. https://doi.org/10.51984/johs.v20i2.1353
Section
Articles