OMCHANGO WA METHALI ZA LAHAJA YA KIMAKUNDUCHI KATIKA MALEZI NA MAKUZI YA WATOTO

Authors

  • Jina Saleh A. M. Saleh Department of Languages and African Studies, Faculty of Languages, University of Sabha

DOI:

https://doi.org/10.51984/johs.v24i2.4247

Keywords:

Kimakunduchi, Lahaja, Methali, Mtoto, Jamii

Abstract

Makala hii imechunguza mchango wa methali katika malezi na makuzi ya mtoto, methali hizo zimekusanywa kutoka kwenye lahaja ya Kimakunduchi kinachozungumza katika Wilaya ya kusini Unguja Zanzibar. Kwa kiwango kikubwa, methali za Wamakunduchi zimezoeleka kuonekana ndani ya vitabu kadhaa vya Kiswahili. Vitabu hivyo viwe vinahusu methali pekee, au hata vile vya hadithi na riwaya za Kiswahili. Katika makala hii, mtafiti amezigawa methali katika sehemu mbali mbali; kama vile:

'Asili/Historia ya jambo', utetezi wa matoto', 'Mahimizo ya kufanya ihsani', 'Methali zenye kufariji', 'Udogo wa mtoto' , 'Athari za mazingira' na mwisho mtafiti amechambua methali za jumla hazikumtaja mtoto wazi wazi.Baada ya mtafiti kuikamilisha kazi yake, amebaini kwamba methali za Wamakunduchi zina mchango mkubwa katika kumleza na kumkuza mtoto, na methali hizo zinasaidia kumwandaa mtoto kukua katika sura inayotakiwa na jamii. Mtafiti ametumia nadharia ya ' Ndani – Nnje' ambayo inasisitiza umuhimu wa kuujua utamaduni wa jamii ambayo mtafiti anataka kuihakikia kazi zake.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2025-09-14

Issue

Section

Articles

Categories

How to Cite

OMCHANGO WA METHALI ZA LAHAJA YA KIMAKUNDUCHI KATIKA MALEZI NA MAKUZI YA WATOTO. (2025). Journal of Human Sciences, 24(2), 143-146. https://doi.org/10.51984/johs.v24i2.4247

Similar Articles

1-10 of 49

You may also start an advanced similarity search for this article.