KUCHUNGUZA UJENZI WA DHAMIRA ZA METHALI KATIKA DIWANI YA SAADANI KANDORO KATIKA MUKTADHA WA JAMII YA KISASA

Authors

  • Ahmed Emhemad Badda Department of Languages and African Studies, Faculty of Languages, University of Sebha

DOI:

https://doi.org/10.51984/johs.v24i2.3582

Keywords:

Diwani, Methali, Dhamira, Jamii ya kisasa, Muktadha wa jamii ya kisasa

Abstract

Wimbi la sayansi na teknolojia limezikumba jamii nyingi, ikiwepo jamii ya Waswahili. Wimbi hili limezifanya jamii kueleza fikra na mitazamo yao kwa njia ya kijigitali jambo ambalo linachochea mabadiliko ya matumizi ya lugha. Katika muktadha huu methali kama sehemu ya hazina ya fasihi simulizi zinakabiliwa na hatari ya kusahauliwa na kupuuzwa, hasa, na kizazi kipya ambacho ndicho kilichokumbatia zaidi usasa katika mawasiliano na burudani. Pamoja na changamoto hizo, methali bado zinaendelea kuwa ni ghala muhimu lenye kuhifadhi ukweli wa maisha, elimu, maadili na utamaduni wa kijamii. Hivyo basi kazi hii inachunguza ujenzi wa dhamira za methali katika diwani ya Saadani Kandoro katika muktadha wa jamii ya kisasa. Methali, kama sehemu ya urithi wa fasihi na utamaduni wa Kiswahili, zimekuwa na nafasi muhimu katika kuendeleza maadili, mitazamo ya kijamii, na mshikamano wa jamii kwa miongo mingi. Hata hivyo, katika zama za sasa zinazokumbwa na mabadiliko ya kijamii, kiteknolojia na kiutamaduni, matumizi na tafsiri ya methali yanahitaji kuchunguzwa kwa mtazamo mpya. Utafiti huu ulitumia mbinu ya uchanganuzi wa kijamii wa fasihi (sociological literary analysis) kuchambua methali zilizotumika katika mashairi ya Kandoro. Methali 19 ziliteuliwa na kuchambuliwa kwa kuzingatia mchango wake katika kujenga dhamira zinazohusiana na maisha ya jamii ya sasa. Nadharia ya kijamii ya fasihi ilitumika kufafanua namna methali hizi zinavyowasilisha mitazamo ya kijamii, mabadiliko ya maadili, haki, usawa wa kijinsia, na mshikamano wa kijamii. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa methali katika diwani ya Kandoro bado zina nafasi muhimu katika jamii ya sasa. Methali hizi hutumika kuhamasisha maadili bora, mshikamano wa kijamii, heshima ya binadamu, na haki za kijamii. Aidha, zimejipenyeza katika mawasiliano ya kisasa kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii, memes, na mijadala ya mtandaoni, hivyo kuendelea kuathiri fikra na mitazamo ya kizazi kipya. Kwa ujumla, utafiti huu umebainisha kuwa methali si tu urithi wa kale bali ni zana hai ya kufundisha, kuonya na kuhamasisha jamii katika zama za sasa. Utafiti unapendekeza kuendelezwa kwa matumizi ya methali katika elimu, fasihi, na mawasiliano ya kijamii ili kusaidia kukuza jamii yenye maadili, mshikamano, na heshima kwa utu wa binadamu.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2025-07-13

Issue

Section

Articles

Categories

How to Cite

KUCHUNGUZA UJENZI WA DHAMIRA ZA METHALI KATIKA DIWANI YA SAADANI KANDORO KATIKA MUKTADHA WA JAMII YA KISASA . (2025). Journal of Human Sciences, 24(2), 27-35. https://doi.org/10.51984/johs.v24i2.3582

Similar Articles

1-10 of 69

You may also start an advanced similarity search for this article.

Most read articles by the same author(s)