Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu

Main Article Content

Ibrahim Elhadi Mohamed Lehmedi

Abstract

Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi  kwa wanafunzi wanaojifunza lugha Kiswahili katika Idara ya lugha na Taaluma za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Sebha kwa muda mrefu, mtafiti aliona kuwa kuna wanafunzi wengi wanakumbana na  matatizo mengi  na ugumu wa kuelewa jinsi na kanuni za uundaji wa vitenzi katika lugha ya Kiswahili. Kwa kuwa mtafiti anaelekea kwenye dhana kwamba tofauti kati ya lugha hizo mbili katika jinsi na kanuni za uundaji wa kauli ya kutendwa ni sababu mojawapo ya kuwepo kwa baadhi ya matatizo na ugumu. Kwa hivyo, mtafiti alichunguza  jinsi ya kubadilisha vitenzi kuwa katika kauli ya kutendwa kisha kuvitumia katika sentensi ili mwanafunzi ajue jinsi na kanuni za uundaji wa kauli ya  kutendwa katika lugha zote mbili Kiswahili na Kiarabu. Ifahamike hapa kuwa utafiti huu unachukuliwa kuwa wa kwanza wa aina yake kwa kuwa ulishughulikia maelezo ya jinsi ya kuunda kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiarabu kwa lugha ya Kiswahili, pamoja na kwamba unachanganya katika kueleza uundaji wa kauli ya kutendwa katika Kiswahili na Kiarabu katika utafiti huo huo. Mwenyezi Mungu akipenda, utafiti huu utakuwa wa thamani si tu kwa wanafunzi wa Kiarabu wanaojifunza lugha ya Kiswahili, bali pia kwa wanafunzi wa Kiswahili wanaojifunza Kiarabu. Pia, utafiti huu utawasaidia katika kujua jinsi ya kuunda kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiarabu na tofauti na lugha ya Kiswahili.  Isitoshe, bali faida itakuwa hata kwa walimu na watafiti wa lugha zote mbili.

Downloads

Download data is not yet available.

Article Details

How to Cite
Lehmedi , I. E. M. (2022). Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu. Journal of Human Sciences, 21(2), 44–50. https://doi.org/10.51984/johs.v21i2.1783
Section
Articles
No Related Submission Found