Maudhui Yanayojitokeza Katika Tamthilia Ya Kaptula La Marx Kupitia Tashtiti

Main Article Content

Abdullah Masoud
Mohamed Omary

Abstract

Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza maudhui ya tamthilia ya kitanzania kaptula la marx kupitia tashtit. Makala haya yanalenga kutathmini maudhui yanayojitokeza kwenye tamthilia hiyo na ni kweli kuwa tamthilia hii ina umuhimu wa kimaudhui na kifani, na inaakisi uhalisia wa mambo katika jamii katika kipindi cha muhimu kwenye historia ya nchi husika. Madhumuni mahsusi ya makala haya ni kuchambua maudhui ya tamthilia ya tajwa ili kuona hatua za maendeleo kimaudhui zilizofikiwa katika tamthilia. Data za utafiti zitakusanywa kwa kutumia mbinu ya upitiaji wa nyaraka maktabani. Na nadharia ya soshiolojia imeongoza makala haya katika uchanganuzi wa maudhui yaliyojitokeza kwenye tamthilia tajwa. Mtafiti amesoma kazi tangulizi katika maktaba za chuo kikuu huria cha tanzania, chuo kikuu cha cairo, chuo kikuu cha dar es salaam na chuo kikuu cha al-azhar. Data hizo zimechambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo kwa madondoo kutoka katika matini ya tamthilia hiyo katika kushadadia hoja.

Downloads

Download data is not yet available.

Article Details

How to Cite
Masoud, A., & Omary , M. (2022). Maudhui Yanayojitokeza Katika Tamthilia Ya Kaptula La Marx Kupitia Tashtiti. Journal of Human Sciences, 21(2), 131–137. https://doi.org/10.51984/johs.v21i2.1989
Section
Articles