Usawiri Wa Mwanamke Katika Utenzi Wa Vitimbi Vya Wanawake

Main Article Content

Husin Hamed Husin Awhida

Abstract

Makala hii yenye madhumuni ya kueleza usawiri wa mwanamke kupitia utenzi wa Vitimbi vya wanawake. Ambapo mwanamke amechorwa ni mtu asiyeaminika, asiyejitambua, asiyejielewa wala kueleweka. Anayeongozwa na utashi wa nafsi yake na mbaya kuliko yote ni ile ya “samaki akioza mmoja kuambiwa wameoza wote”. Kwa kosa la mwanamke mmoja kuchukuliwa ni kosa la wanawake wote. Tatizo lililojitokeza ni kuona  jinsi mwanamke alivyochorwa  kuwa ni mtu anaejikomboa kutokana na  mfumo mbaya wa ubabe dume katika jamii. Lakini mbinu au njia iliyotumika ni ya udhalilishaji kabisa. Kwani badala ya mwanamke huyo kuonekana amejikomboa kwa kutumia njia zinazokubalika kama vile; ya mazungumzo (siasa). Matokeo yake mwanamke huyo kuonekana  amedhalilika zaidi. Katika kujipatia ukombozi wake. Mbinu zilizotumika katika makala hii ni ya maktabani. Kwa kuipitia matini husika na kuiona jinsi ilivyomsawiri mwanamke.  Na mwanamke huyo kutambulika ni mtu wa namna gani katika jamii anayoishi. Makala hii imeeelezea historia ya mwandishi kwa ufupi, dhana ya usawiri. Nadharia iliyotumika katika makala hii ni nadharia ya mtazamo kike. Kwa lengo la kuonyesha jinsi gani mwanamke anahitaji kujikomboa dhidi ya ukandamizwaji wa mwanamme. Kwa umuhimu wa uchambuzi wa makala hii, imeeleza kuwa mwanamke ni mtu wa kuenziwa pamoja  na kuthaminiwa  na sio kudhalilishwa na kubandikiziwa kashfa juu ya kashfa ni hasara iliyoje. Kwani kila mwanaadamu awe mwanamke au mwanamme ana uhusiano wa namna moja au nyengine na mwanamke. Hivyo kumdhalilisha au kumgandamiza mwanamke ni sawa na mtu kujidhalilisha mwenyewe.

Downloads

Download data is not yet available.

Article Details

How to Cite
Awhida , H. . H. . H. . . (2021). Usawiri Wa Mwanamke Katika Utenzi Wa Vitimbi Vya Wanawake. Journal of Human Sciences, 20(2), 101–105. https://doi.org/10.51984/johs.v20i2.1767
Section
Articles
No Related Submission Found