ATHARI ZA TEKNOLOJIA KATIKA UKUZAJI WA LUGHA YA KISWAHILI " UCHUNGUZI KIFANI "

Authors

  • Emhemad Abdallah Alhabib Department of African Languages and Studies, Faculty of Languages, Sebha University
  • Jalgham Abuazuom Emhemmed Ali Department of African Languages and Studies, Faculty of Languages, Sebha University

DOI:

https://doi.org/10.51984/kr9zz707

Keywords:

Kiswahili, Teknolojia, Ukuzaji wa Lugha, Upangaji Lugha, Mitandao ya Kijamii

Abstract

Utafiti huu unachunguza nafasi ya teknolojia katika ukuzaji wa lugha ya Kiswahili kwa kuangazia maeneo ya upangaji lugha kama uteuzi, usanifishaji, uenezaji, uendelezaji na tathmini. Licha ya maendeleo makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika karne ya ishirini na moja, tafiti nyingi zimejikita zaidi katika historia na fasihi ya Kiswahili huku zikipuuzia mchango wa teknolojia katika kukuza lugha hii. Utafiti huu umetumia mbinu ya kimaelezo na mchanganyiko, ukiunganisha hojaji, mahojiano, uchambuzi wa nyaraka na uangalizi ili kupata data kutoka kwa walimu, wanafunzi na wataalamu wa lugha. Matokeo yanaonyesha kuwa teknolojia imekuwa chombo muhimu cha kukuza Kiswahili kitaifa na kimataifa kupitia mitandao ya kijamii, vyombo vya habari, fasihi mtandaoni na programu za lugha. Hata hivyo, changamoto kama kuchanganywa kwa lugha (code-switching), matumizi ya Kiswahili kisicho sanifu, tafsiri zisizo sahihi na kupotea kwa baadhi ya vipengele vya utamaduni wa Kiswahili zimejitokeza. Utafiti unahitimisha kwamba teknolojia ni chombo chenye manufaa makubwa katika kukuza Kiswahili, lakini inahitaji mikakati thabiti ya kisera na kitaaluma ili kulinda ubora na uthabiti wa lugha hii.       

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2026-02-18

Issue

Section

Articles

Categories

How to Cite

ATHARI ZA TEKNOLOJIA KATIKA UKUZAJI WA LUGHA YA KISWAHILI " UCHUNGUZI KIFANI ". (2026). Journal of Human Sciences, 25(1), 131-138. https://doi.org/10.51984/kr9zz707

Similar Articles

81-90 of 165

You may also start an advanced similarity search for this article.